Sunday, 29 April 2018

ULIMWENGU WA MOVIES....
Wale wapenzi wa film za Drama kali nyingine hii inaitwa DISOBEDIENCE (KUKOSA HESHIMA) imeachiwa tar 27 April 2018 iliyoigizwa na mwanadada Rachel Weisz raia wa kiingereza akijulikana kwa jina maarufu la Ronit Krushka.kua wa kwanza kuipata na fuatilia page yetu kupata dondoo zaidi.








FT: SIMBA 1-0 YANGA, KUTOKA UWANJA WA TAIFA mnyama aunguruma.

SIMBA  wanaibuka kidedea na kujikita kileleni kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu ya vodacom kwa kupata alama 3 muhimu kwa goli lililofungwa na Erasto Nyoni dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza.



VIDEO: MASHABIKI WA SIMBA KIMEWAKA MSIMBAZI WAWASHA MOTO!!



MASHABIKI wa Simba wameendelea kutamba katika harakati za kutetea ubingwa na watani wao wa jadi Yanga katika mchezo wao leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Mashabiki hao wameonekana kujiamini kila shabiki akisema kuwa simba itachukua ubingwa na itawafunga watani wao katika mchezo wa jumapili. Simba na Yanga zitashuka dimbani katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Saturday, 28 April 2018

April ,28 2018

NAFASI ZA AJIRA JKT KWA MWAKA WA FEDHA 2017/ 18

JESHI la Polisi Tanzania limetangaza nafasi za ajira kwa mwaka wa fedha 2017/ 18 kwa vijana waliopo kwenye kambi za JKT/JKU ambao wamemaliza mafunzo ya awali katika Operationi Kikwete na Operesheni Magufuli
WATATU WAFARIKI KWA AJALI YA BASI Kagera

WATU watatu wamefariki dunia papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kugongwa na Basi la Kampuni ya Frester lenye namba za usajili T 720 DEV eneo la Katongo, Kata ya Rulanda wilayani Muleba mkoani Kagera leo Asubuhi Aprili 28, 2018 ambapo basi hilo lilikuwa likitokea Bukoba kuelekea Mwanza.

Vijana hao wamekumbwa na ajali hiyo wakati wakiwa njiani kwenda Madrasa huku miili yao ikiwa haijatambulika.

Kwa mujibu wa abiria waliokuwa kwenye basi hilo wamesema, chanzo cha ajali ni dereva wa basi alipokuwa akimkwepa mwendesha bodaboda hivyo kuwaparamia vijana hao akiwemo huyo bodaboda na kusababisha basi hilo kupinduka.
Abiria wote waliojeruhiwa kwenye basi hilo wameokolewa na wenzao huku zikifanyika jitihada za kuwapeleka Kituo cha Afya Kaigara na Hospitali ya rufaa wilayani Muleba.
April 28 ,2018

RAIS MAGUFULI AMLILIA ABBAS KANDO


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia marehemu kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa.

INIESTA ATANGAZA Kuondoka BARCELONA

UHISPANIA: Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Soka ya Barcelona, Andres Iniesta (33) ametangaza kuondoka klabuni hapo ifikapo mwisho wa msimu huu 2017/18.
Kiungo huyo raia wa Uhispania aliyeichezea klabu hiyo kwa miaka 22 na kushinda mataji 31 amesema hataweza kucheza dhidi ya Barcelona atakapoondoka klabuni hapo.


Iniesta maarufu kama ‘Magician’ ni mchezaji pekee kuwahi kuwa mchezaji bora (Man of the match) katika fainali ya EUROs, fainali ya Kombe la Dunia na fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kiuongo huyo bora duniani anatarajiwa kwenda kukipiga China ambapo inadaiwa atalipwa mkwanja mara mbili ya ule anaolipwa Barcelona. Aidha, Iniesta amesema hataki tena kucheza Soka Bara la Ulaya kwa sababu atakutana katika mechi na timu yake iliyomlea Barcelona jambo ambalo anaona kwake haitakuwa vyema kupambana na mlezi wake.

TCU: HELWAN UNIVERSITY SCHOLARSHIP CALL FOR APPLICATION FOR THE ACADEMIC YEAR 20

1.0 Call for Application Applications are invited from qualified Tanzanians for 7 scholarships (5 for Undergraduate, 1 for Masters an...